Siku ya kwanza: SAFARI YA IDARA YA INJILI NA MISHENI AICT “BURUNDI LIVE”

Ziara ya watu 16 wa kikundi cha Injili na Misheni  cha AICT  tarehe 1-5-2014, saa 10 alfajili walianza safari ya kwenda Nchi ya Burundi kuona uwezekano wa kuanzisha kanisa la AIC Burundi.  Wana kikundi walio kwenda ni:

 (1) David Emanuel -Mpiga picha za video
(2) Grace Shunashu -Mhazini msaidizi
(3) Mwinj. Benjamini kafula -Buzuruga
(4) Gereshom Fereshi -Mtumishi AIC Ufundi
(5) Paul Buyemba  -Mtumishi AIC Inland Press
(6) Abigael Zebedayo -Mwimbaji Paradiso Choir AIC Buzuruga
(7) Mch. Charles Mabisa -AIC Makongoro
(8) Mwinj. Esther Shija -Mjumbe kamati ya Injili na Misheni
(9) Joseph Masunzu Kuzenza -Mzee wa kanisa AIC Shinyanga
(10) Mwinj. Yohana Bwire -Mratibu wa Injili na Misheni dayosisi ya Pwani
(11) Mch. Charles Sanagu - Mch. wa Changanyikeni Dar
(12) Mch. Emanuel Makunza -AIC Mtwara
(13) Mch. Mussa Hezeron -AIC Magomeni
(14) Mch. Zabroni Kashinje -AIC Misungwi
(15) Mch. Samwel Lupilya -AIC Buzuruga
(16) Mwinj. Stephen Kapongo -Mratibu Mkuu wa Idara ya Injili na Misheni AICT

Safari ilianzia  kituo cha Emaus Makongoro Mwanza, na kufika AICT Dayosisi ya Geita saa 3.20 asubuhi  mahali ambapo Idara ya Vijana AICT Dayosisi ya GEITA iliwakarimu chai na maji ya kunywa na safari ya Burundi ikaendelea.

Mungu akatenda muujiza kikundi  kilipofika eneo la K9 wilaya ya Ngara mnamo saa 6 mchana.  Mpwa wake na Ndg. Gereshom Fereshi anayeitwa Mwalimu Pius Radislaus  alikikaribisha kikundi cha Injili na Misheni nyumbani kwake na kukikarimu chakula cha mchana na vinywaji. Kabla ya kuondoka nyumbani kwake kiongozi wa msafara Mwinjilisti Stephen Kapongo akamuomba Mch. Samwel Lupilya kumbariki mtoto mchanga wa familia ya Mwalimu Pius Radislaus.

Kikundi  kilifika Kabanga mpakani mwa Tanzania na Burundi  saa 10.20 jioni na baada ya kukamilisha taratibu zote za uamiaji kikundi kikaruhusiwa kuingia nchi ya Burundi.

Safari iliendelea  na iliwachukua takribani masaa maNne zaidi kufika rango kuu la kuingia  jiji la Bujumbula. Hii ni sehemu ambapo mwenyeji wao Mwinjilisti Kiongozi wa Burundi Ndg. Manjondi Ezechiel aliwapokea mnamo saa 4.20 usiku. Alikiongoza kikundi hadi kanisani wakafanya ibada ya kumshukuru Mungu kwa wageni kusafiri na kufika salama. Pia viongozi wenyeji wakapata fursa ya kujitambulisha kwa wageni. Badae wageni wakapewa chakula  cha usiku na kupumzika ili kujiandaa na kazi ya siku ya pili..

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found