Maaskofu wahudhuria mazishi ya Mzee Andrew Yohana Kinuno

Askofu Mkuu Silas Kezakubi, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tabora, na Askofu John Kanoni Nkola wa Dayosisi ya Shinyanga hivi karibuni walihudhuria ibada ya mazishi ya Mkristo mjini Tabora. Askofu John Kanoni Nkola alihuri katika mazishi hayo ya Mzee Andrew Yohana Kinuno ambaye alifariki tarehe 10-8-2015 na kuzikwa 12-8-2015. MzeeKinuno alikuwa mstari wa mbele katika shughuri nzima ya uanzishwaji wa AICT Dayosisi ya Tabora hapo 2006 na hivyo kuwa karibu sana na viongozi hao wa kanisa. Katika mahubiri yake, Askofu Nkola aliwaasa wakristo wafuate mfano wa Mzee Kinuno wa kubaki katika Imani licha ya changamoto nyingi za maisha zinazowakabili katika wakati huu ambazo alizilinganisha na birika lenye moto.

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found