Askofu Mkuu Atembelea Kituo cha AICT Vijana-Geita

Askofu Mkuu wa AICT Silas Kezakubi alifanya ziara ya kikazi kwenye kituo cha vijana AICT kilichomo katika mji wa Geita. Ziara hiyo ambayo ilianza Novemba 10 na kukamilika 11, 2015 ilielezwa kuwa ndiyo ya kwanza kufanywa na Askofu Mkuu aliyeko madarakani katika historia ya kituo hicho. Katika ziara hiyo, Askofu Mkuu aliiagiza Bodi kukamirisha ujenzi wa upanuzi wa nyumba ya wageni ambao umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja hivi sasa bila ya kukamilika. Aliagiza ujenzi huo ukamilike kabla ya mwezi Augusti 2016 au sivyo kanisa litachukua hatua. Aidha alionyesha mshango kuwa idara hiyo hivi sasa inaendeshwa na wazalendo takribani kwa miaka arobaini lakini mishindwa kuongeza raslimali hivyo kuendelea kutumia zile tu zilizojengwa na wamisionari.

Kituo cha vijana cha Geita, ambacho ndiyo mhimili mkubwa katika uendeshaji wa shughuri za idara ya vijana katika kanisa hilo kutokana na uzalishaji wake, kinavyo vitengo vikubwa vitatu. Ketengo cha kwanza ni nyumba ya wageni (hostel) ambayo imekuwa chanzo cha mapato kwa idara hiyo tangu miaka ya 70. Nyumba hii, ambayo ilijengwa kwa msaada wa makanisa ya Ujerumani imeendelea kutoa huduma kwa wageni wengi wanaokuja katika mji wa Geita. Kitengo hiki kimekuwa kikifanyiwa upanuzi zaidi ya mwaka hivi sasa.

Kitengo cha pili ni karakana ambayo inahusu ufundishaji wa kutengeneza vifaa vya mbao (furniture) na vifaa vya chuma. Kitengo hiki kimesajiriwa na VETA kutoa mafuzo ya ufundi kwa vijana. Hadi sasa kinao wanafuzi kumi katika sehemu zote mbili.

Kitengo cha tatu ni kile cha tiba asili (ANIMED) na kiwanda kidogo cha kusindika mafuta. Kitengo hiki, ambachi kwa sasa kinaendeshwa na mmishenari bado kichanga. Hata hivyo kinaendelea kufahamika. Kwa kulingana na 

maelezo ya uongozi wa kitengo, madhumuni yake ni kutibu kwa kutumia dawa za asili na kuwafundisha wateja  wao na kuwahimiza kupanda miti hiyo kwa tiba yao na jirani zao.

Kituo pia kinalo shamba zuri kwa ajili ya kilimo ambalo, hata hivyo, mazo yake hayako katika hali nzuri. Kiongozi huyo wa kanisa aliagiza uongozi utafute mtalaam wa kilimo wa kutoa ushauri ili shamba hilo lipate kutumika vizuri.

Awali, akitoa taarifa ya kituo hicho cha vijana, Mratibu wa idara ya vijana wa kanisa Mchungaji Abel Lugayila, alisema nyumba ya wageni imewezesha kupata fedha za kuwalipa waratiby wote wa idara hiyo walioko katika Dayosisi zote sita. Aidha, Alisema mradi wa karakana umewezesha vijana wa kanisani na wale wa nje kupata ajira. Akichangia katika kikao hicho cha pamoja, mmoja wa wana bodi wa kituo hicho alitahadharisha juu ya kukaribisha baadhi ya watu kupanga katika majengo na maeneo ya idara hiyo bila mikataba mizuri.

Bodi pamoja na wafanyakazi walimshukuru Askofu Mkuu kufanya ziara hiyo na kikao hicho cha pamoja kilihitimishwa kwa sala ya mtu mmoja.

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found