Askofu Charles Salala Afanya Ziara ya Kikazi Katika Dayosisi ya Tabora

Askofu Charles Salala wa AICT Dayosisi ya Pwani, akiwa ameambatana na mkewe, hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi katika AICT Dayosisi ya Tabora. Akiwa katika ziara hiyo, ambayo ilianza December 19, 2015 na kukamilika January 4, 2016, Askofu Salala alibariki na kuwaingiza kazini wachungaji wawili ambao ni Mchungaji Simon Kuhanda wa kanisa la Usevya katika Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Mulele na Mchungaji Daniel Malale wa kanisa la Mwamapuli katika Mkoa huo huo na Wilaya hiyo hiyo. Aidha, katika kipindi hicho chote, Askofu alihubiri katika makanisa 12 na kuweka mawe ya msingi kwenye majengo 6. Kiongozi huyo wa kanisa alihitimisha ziara yake kwa kubariki ndoa kumi na moja katika kanisa la Katavi lililoko kwenye mji wa Mpanda Mkoani katavi.

Wakizungumzia tukio hilo, baadhi ya wakristo katima eneo alilolitembelea Askofu Salala walielezea furaha yako kubwa kuona jinsi viongozi wao wanavyoweza kushirikiana katika kuliogoza kanisa. “Tumefurahi mno kuona kuwa Askofu wa Pwani anaweza kuja kutuhudumia na bila shaka wa Tabora anaweza kuhudumia Pwani”, mama mmoja alisikika akisema.

 

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found