Askofu Dr Nkola Aanza Rasmi Mchakato wa Kustafuu

Bishop Kanoni Daniel Nkola

Askofu Dr. John Kanoni Nkola wa Dayosisi ya Shinyanga, AICT, ametangaza rasmi kuanza kwa mchakato wa mwaka mmoja wa kustaafu uongozi. Tamko hilo alitoa kwenye ibada maalum ya kuuzindua mchakato huo iliyofanyika Jumapili ya tarehe 5 Juni, 2016 katika kanisa kuu la Kambalage mjini Shinyanga. Akitangaza kuanza kwa mchakato huo, Askofu Dr. Nkola alisema, “Miaka 23 iliyopita, Bwana, kupitia uongozi wa kanisa, alinipatia jukumu la kuongoza Dayosisi hii. Na kazi hiyo nimeifanya kwa kumtii na kumwogopa Mungu.” Aliwashukuru  wakristo wote, hususani wa kanisa  kuu, kwa ushirikiano  mzuri na mkubwa waliompatia katika kipindi chote hicho. Aliongeza, “Busara yenu na upendo wenu hakika vilinifanya niifurahie kazi hii.” 

Bishop Silas Kezakubi

Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Silas Kezakubi ndiye alikuwa mhubiri katika ibada hiyo. Katika mahubiri yake, Askofu Kezakubi aliwahimiza wakristo wote kushrikiana na uongozi wa kanisa hilo katika kuweka njia madhubuti za kuwatunza watumishi wa kanisa hapo wanapostaafu. “Mungu hafurahii kuona watu waliotoa maisha yao kumtumikia Yeye, na wakatumika hadi kuishiwa nguvu, baadaye wanapostaafu wanaishi kwa machozi.” Aliongeza kuwa utaratibu uliopo kwa sasa ni wastaafu hao kutunzwa na Pastorate au Doyosisi wanamoishi. Alibainisha kuwa, “utaratibu huo umeshindwa kwani pastorate nyingi hazina uwezo wa kumtunza mtumishi anayezihudumia na pia kumtunza mstaafu”. Alieleza kuwa njia nzuri ilikuwa kuwekeza katika majengo kwenye viwanja vyetu na kuweka kando sehemu ya mapato ya majengo hayo kwa kuwatunza wastaafu.

Bishop Nkola akiwa na Katibu wa Dayosisi ya Shinyanga

Awali, Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Mchungaji Jacob Pambana alitoa ufafanuzi juu ya namna kanisa litakavyomuaga wakati wa kustaafu. 

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found