BARAZA LA UTENDAJI LAPATA WAJUMBE WAPYA

Kushoto ni Mchungaji Joseph Mayala na Kulia ni Ndugu Ndaki P. Munyeti. 

Baraza la Utendaji la Sinodi Kuu litakutakuwa na kikao chake cha kawaida tarehe 22 na 23 March 2018 likiwa na wajumbe wawili wapya. Wajumbe hao, ambao Baraza hilo liliteua kuwa wenyeviti wa idara za kanisa tangu mwezi August 2017, ni Mchungaji Joseph Mayala na Munyeti.

Mchungaji Joseph Mayala  (pichani)aliteuwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Theologian a Mafunzo ya Biblia. Idara ambayo inasimamia vyuo vyote vya kanisa na mafunzo mengine ya Biblia. Mchungaji Mayala, ambaye ni mmoja wa wajumbe vijana, anaingia katika Baraza hili akiwa na uzoefu mkubwa kutoka katika mashirika makubwa aliyofanya kazi nayo. Mashirika hayo ni pamoja na Barclays, Compassion International na hivi sasa anafanya na shirika laata sasa World Vision. Mchungaji Mayala hata sasa ni mjumbe wa Bodi ya Africa International University (AIU) ambayo zamani iliitwa NEGST. Mara tu alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hii, alianza juhudi za kuleta vitabu vya kutosha kwenye Chuo cha Theologia cha Nasa na hata kutafuta uwezekano wa kukifanya kifanye kazi na AIU ili kuinua taaruma.

Mjumbe mpya wa pili ni Ndugu Ndaki P. Munyeti  ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Mawasiliano.  Yeye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  Tanais ambayo makao makuu yake yako Dar Es Salaam. Yeye amefanya kazi na makampuni makubwa. Ni mtalaam wa kutoa ushauri katika viwanda. Anatoa ushauri kwenye makampuni ya nchini nay a nje ya nchi, kazi ambayo imemfanya atembelee nchi nyingi.

 

   Kanisa la AICT liko katika harakati za kuanzisha kituo cha redio na pia kituo cha TV. Ndugu Ndaki P. Munyeti ndiye Mwenyekiti wa Bodi iliyoundwa ili kusimamia uanzishwaji wa vyombo hivyo vya mawasiliano.

Mapendekezo ya Mabadiriko ya Katiba

Moja ya mambo muhimu yanayotarajiwa katika kikao hiki ni kupanga tarehe ambayo Sinodi Kuu itakaa ili kupitisha au kukataa mapendekezo ya mabadiriko ya Katiba ya kanisa. Likiwa sasa limeingia karne ya pili tangu lilipoanzishwa (1909), wakristo wa kanisa hilo wametoa mapendekezo mengi ya mabadiriko ya Katiba ili kulifanya kuwa imara katikati ya changamoto mpya zilizomo katika jamii zote. Baadhi ya mapendekezo hayo yanalenga kuimarisha utawala (governance) kwa kuongeza majukumu ya mabaraza na kuongeza idadi ya vikao. Kwa upande wa nidhamu kwa viongozi, wakristo wengi wamependekeza pawepo na chombo ambacho kitashughurikia jambo maadili kwa watumishi wa kanisa na hasa uwakili wa mali za kanisa.

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found