//social-icons

Kanisa Kuu Dayosisi ya Tabora Lamwaga Askofu Mstaafu Dr Peter Kitula

Posted on 09/09/2018 at 17:44

Askofu Mstaafu Dr Peter Kitula amepengezwa na Kanisa Kuu la Tabora kwa utumishi wake wa miaka mingi.Baba Askofu Kitula alistaafu rasmi tarehe 5 August, 2018 katika viwanja vya ofisi ya Dayosisi ya Mara na Ukerewe vilivyoko maeneo ya Bweli mjini Musoma. Kabla ya kustaafu, alitembelea kanisa Kuu la Dayosisi ya Shinyanga na lile la Dayosisi ya Mwanza kwa madhumuni ya kuagana na waumini.

Katika mahubiri yake yaliyojikita katika kitabu cha Luka 24:44-53 Askofu Kitula alikazia mambo matatu muhim katika maisha ya mkriato. “Jambo la kwanza”, alisema, “ni kufunuliwa akili ili kuielewa Injili”. Injili aliifafanua kuwa ni kuteswa, kufa na kufufuliwa kwa Bwana Yesu Kristo. Aliongeza kuwa pale mtu anapofunuliwa kumfahamu Kristo dipo anapobeba jukumu la kuwa shahidi wake Yesu.Kukaa kanisani miaka mingi au kuzaliwa katika nyumba au ukoo wa kikristo peke yake havitoshi. Mtu lazima afunuliwe kumfahamu Kristo dip awe mfuasi wa Kristo wa kweli.

Jambo la pili, Askofu Kitula alisema ni lazima mkristo aishi maisha ya kumshudia Kristo. Maisha ya mkristo wa kweli yanazungumza habari za Kristo anayeokoa. Tena maisha ya Mkristo ni lazima yazungumze juu ya ondoleo la dhambi linalopatikana kwa Kristo pekee. Kila mwanadamu anahitaji kusamehewa na kupata ondleo la dhambi.Jambo la tatu, tunasoma katika fungu hilo kuwa Bwana Yesu aliinua mikono yake akawabariki.

Kanisa la Tabora hufanya ibada mbili kwa kulingana na mahitaji wa wakristo wake. Kuna wale ambao huhitaji ibada ya mapema ili waweze kwenda kwenye majukumu. Ibada hiyo ya kwanza huanza saa 1.00 na kusha saa 3:30 asubuhi na ibada yap ili huanza saa 4:00 hadi saa 6:30. Askofu Mstaafu Peter Kitula ndiye aliyekuwa mhubiri katika ibada zote hizo mbili. Wakristo waliofanikiwa kusikika wakizungumzia mahubiri hayo walielezea jinsi yalivyosaidia katika kutafakari maisha yao ya kikristo mbele ya jamii.

 

Post Your Comment

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register