KUPIGA KURA KUPITISHA MAPENDEKEZO YA KUINGIZWA KWENYE KATIBA YA KANISA

Wajumbe waliohudhuria kwenye Vikao vya Sinodi Kuu ya AICT iliyokaa tarehe 9 Septemba 2021 walipata fursa ya kupiga kura kupitisha mapendekezo mapya ya kuingizwa kwenye katiba ya Kanisa. Zaidi ya wajumbe 800 walihidhuria na kupata fursa ya kupiga kura mapendekezo mapya. kulikuwa na mapendekezo 29 ambayo yalikuwa yanapigiwa kura katika kikao hicho. 

Mapendekezo ya Kuingizwa katika Katiba ya AICT ni kama ifuatavyo

 1. Kuzuia Dayosisi kuwa na Katiba yake.
 2. Kufutwa kwa Baraza la Fedha na badala yake kuanzishwa Kamati ya Fedha na Ukaguzi.
 3. Kubainishwa Mavazi stahiki na wajibu wa Muumini wa AICT.
 4. Wanawake kuruhusiwa kuwa wazee na Wahudumu wa Kanisa.
 5. Katibu Mkuu wa Dayosisi kuwa Katibu wa Dayosisi.
 6. Kuanzishwa Baraza Maalum la Maaskofu wa AICT.
 7. Kubadili jina la ngazi ya Chalo kuwa Jimbo.
 8. Mfumo mpya wa fedha na Mawasilisho.
 9. Mfumo mpya wa Ajira na ulipaji wa Maslahi kwa Watumishi wa AICT.
 10. AICT Kugharamia Kozi za Wachungaji na Wainjilisti
 11. Kuwekwa Utaratibu wa Kujaza nafasi ya Askofu Mkuu au Makamu wa Askofu Mkuu nafasi ikiwa wazi kabla ya kumaliza muda wake.
 12. Nguvu ya pamoja katika uwekezaji.
 13. Kanisa kutambua ushiriki wa Diaspora wake na kuwashirikisha kwenye Ibada na shughuli za Kanisa
 14. Muundo mpya wa AICT, Kwaya na taratibu za uendeshaji wake.
 15. Utaratibu wa kuhudumu kwa Watumishi Wastaafu wa AICT.
 16. Kuanzishwa kwa Kurugenzi za AICT na majukumu yake.
 17. Muda wa mafundisho ya ndoa usipungue siku ishirini na moja.
 18. Kubainishwa kwa maeneo ya mazishi kwa Viongozi wa kiroho wa AICT.
 19. Mtu atakayemwamini Yesu Kristo atabatizwa na kuingia katika ushirika wa AICT (isipokuwa Ushirika Mtakatifu na uongozi) na ataendelea na mafundisho ya Katekisimu kwa muda wa miezi sita.
 20. Kutenganisha Katiba na Sheria (kwa sasa zinatwa Kanuni)
 21. Utaratibu mpya wa utatuzi wa migogoro ndani ya AICT.
 22. Kubadilika kwa muda wa Uchaguzi Mkuu wa AICT kutoka miaka minne (4) na kuwa miaka mitano (5) na itakuwa kwa ngazi zote za uongozi.
 23. Katibu Mkuu kiongozi kuitwa Katibu Mkuu na kuwa pia Katibu wa Sinodi Kuu na Baraza la Utendaji la Sinodi Kuu.
 24. Askofu Mkuu kufanyia kazi Makao Makuu ya AICT na kuwa Askofu wa Dayosisi yaliko Makao Makuu ya AICT.
 25. Askofu Mkuu Msaidizi kuitwa Makamu wa Askofu Mkuu ambaye pia kituo chake cha kazi kitakuwa kwenye Dayosisi aliyopangiwa.
 26. Kuwepo utaratibu maalum wa Uhamisho wa Maaskofu na Makatibu wa Dayosisi.
 27. Matoleo ya Fungu sasa kuitwa Ada ya Mkristo ya mwaka.
 28. Ukomo wa kazi ya Uaskofu
 29. Utaratibu wa kumvua Askofu Uaskofu wa AICT

 

na katika mapendekezo yote mapendekezo 26 yalipitishwa na mapendekezo 3 hayakupitishwa mapendekezo ambayo hayakupitishwa ni

 1. Wanawake kuruhusiwa kuwa wazee na Wahudumu wa Kanisa.
 2. Muda wa mafundisho ya ndoa usipungue siku ishirini na moja.
 3. Mtu atakayemwamini Yesu Kristo atabatizwa na kuingia katika ushirika wa AICT (isipokuwa Ushirika Mtakatifu na uongozi) na ataendelea na mafundisho ya Katekisimu kwa muda wa miezi sita.

 

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
  No comments found