Pastor Aaron Isilyumu Malyuta

Aaron Isilyumu Malyuta profile Pastor

  • Full names:
    Aaron Isilyumu Malyuta
  • Church:
    KAMBARAGE
  • Pastorate name:
    Kambarage
  • Diocese name:
    SHINYANGA
  • Date Of Birth:
    30/5/1948
  • Married to:
    Florence Seleman
  • Joined Pastorship in:
    2000

Biography

Nilianza kusoma shule ya datasa la kwanza, 1957 huko Kwimba na kumaliza darasa la nne na kujiunga middle school Buyogo 1961. Nilihitimu darasa la saba, 1964 na kujiunga na shule ya Sekondari ya Shinyanga nilihitimu kidato cha nne mwaka 1968. Nilienda chuo cha ualimu Marangu Moshi 1969-1970. Nilijiunga na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria na baada ya hapo niliajiriwa kazi ya ualimu katika shule ya msingi wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza. Nimefundisha shule mbalimbali na nyadhifa kama mwalimu mkuu na mratibu wa elimu wa kata. Pia nilichukua mafunzo ya elimu maalumu huko Tabora na kuwa mwalimu wa viziwi na kufundisha shule ya viziwi, Mugeza Bukoba. 

Nilimwamini Yesu 1957 na kubatizwa 1961 huko Kijima. Nilitumika kanisani kama mzee wa Kanisa sehemu ambayo nilikaa kikazi. Mwaka 1989 nilienda kusoma chuo cha Biblia huko Nassa (NTC) hadi 1992 nilipotumwa kufundisha shule ya Biblia Katungulu. Mwaka 2002 nilihama na kuwa Mchungaji wa Buginza dayosisi ya Shinyanga na baadae kuhamia AICT Bariadi. Nilichaguliwa kuwa Mchungaji msaidizi wa Askofu mwaka 2015 dayosisi ya Shinyanga na kuhamia kanisa la AICT Kambarage, kwa sasa pia ni mwenyekiti wa idara ya injili na Misheni wa kanisa letu AICT.

Posts

    No posts made yet by this leader

Photos

Mchungaji Paul Mabula Kengele akiwa na mke wake.