
Ufunguzi wa madarasa na ofisi ya chuo cha uuguzi AICT Kolandoto, ulifanyika tarehe 31/10/2014 katika eneo la Chuo cha Uuguzi cha Kolondoto, dayosisi ya Shinyanga. Mgeni rasmi alikuwa Askofu Mkuu wa AICT Silas Kezakubi, ambaye alifuatana na Katibu Mkuu wa AICT Mch Zakayo Bugota. Uzinduzi ulihudhuliwa pia na viongozi wa Idara ya Afya kama vile Mwenyekiti wa Bodi, Mkurugenzi mkuu Dkt Shadrack Watugala, Mkuu wa Chuo cha uuguzi Kolandoto Ndg Daudi Malimi, pamoja na madkitari, wauguzi, waumini wa AICT na watu mbalimbali.