
Mahafali ya kutoa vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya uuguzi katika chuo cha Kolandoto yalifanyika tarehe 31/10/2014 Kolandoto Shinyanga. Vyeti vilitolewa na Askofu Mkuu, Silas Kezakubi kwa wahitimu wote wa mafunzo hayo. Sherehe hio ilihudhuriwa na Katibu Mkuu, Mwenyekiti wa bodi ya afya, Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Mkuu wa Chuo, wafanyakazi, viongozi na watu mbalimbali.