
Askofu Mkuu Silas Kezakubi, ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tabora, na Askofu John Kanoni Nkola wa Dayosisi ya Shinyanga hivi karibuni walihudhuria ibada ya mazishi ya Mkristo mjini Tabora. Askofu John Kanoni Nkola alihuri katika mazishi hayo ya Mzee Andrew Yohana Kinuno ambaye alifariki tarehe 10-8-2015 na kuzikwa 12-8-2015. MzeeKinuno alikuwa mstari wa mbele katika shughuri nzima ya uanzishwaji wa AICT Dayosisi ya Tabora hapo 2006 na hivyo kuwa karibu sana na viongozi hao wa kanisa.