//social-icons

Faragha ya Maaskofu na wake wao photos

Faragha ya Maaskofu na wake wao
Hapa Mchungaji Tonny Surgent, mhubiri katika faragha ya maombe hiyo akielezea jambo wakati wa kipind Jengo kuu la kituo cha Sanga Sanga nje kidogo ya mji wa Morogoro. Katika picha hii Mchungaji Tony Swanson ambaye ndiye Mkuruganzi wa kituo cha Sanga Sanga anawaonye m
Hivi karibuni maaskofu wote sita wa Africa Inland Church Tanzania pamoja na wake zao walikuwa na faragha ya maombi katika kituo cha Sanga Sanga kinachoendeshwa na Dayosisi ya Pwana ya kanisa hilo. Faragha hiyo ya siku tatu ilikuwa ya maandalizi ya Mkutano wa kuadhimisha miaka 20 ya dayosisi hiyo ya Pwani. Maombi hayo ya faragha yalianza Novemba 23 hadi 25, na tarehe 26 maaskofu hao pamoja na wenzi wao walisafiri kwenda Dar-es-Salaam tayari kwa kuanza kwa maadhimisho kesho yake. Mhubiri katika wa faragha hiyo alikuwa ni Mchugaji Tonny Surgent kutoka Wingereza. Wakati wa kuhitimisha faragha hiyo, mgeni huyo alisisitiza umuhimu wa watumishi wa kada mbali mbali katika kanisa, na hasa walioko katika maeneo ambayo kanisa bado ni change, kupata mafunzo ya kazi zao. Aliahidi kuendelea kuiombea Dayosisi ya Pwani na kanisa zima la Africa Inland Church Tanzania kuwa na vituo vya kutolea mafunzo ya namna hiyo.