“Siku ya pili” Kikundi cha Injili na Misheni kilifundisha Imani ya Kanisa la AICT Nchini Burundi

Mafunzo juu ya imani ya kanisa la AICT.
Siku ya tarehe 2/05/2014 saa 4 asubuhi “program” ya Idara ya Injili na Misheni ili anza kazi  rasmi  katika kanisa la AIC Burundi.  Zamani liliitwa kanisa la "ENGLISE EMMANUEL MIRACLE CENTER"
 Baada ya ibada fupi ya asubuhi Uongozi wa AIC Burundi zamani "Kanisa la ENGLISE EMMANUEL MIRACLE CENTER"  wakajitambulisha kwa wangeni kama ifuatavyo:-

1. Manjondi Ezechiel- Mwinjilisti kiongonzi
2. Nicitegetse Pascal-Mwinjilisti msaidizi kiongonzi
3. Nkeshimana Marc-Katibu
4. Minani Egiole-Mhazini
5. Kakozi Martin- Mwinjilisti wa kanisa na mshauri

Katika utambulisho huo; Mwinjilisti kiongozi-Manjondi Ezechiel alimtambulisha Mwinjilisti kiongozi Ndg. Sharamba Augustini Akasante kutoka Congo. Alisema huko nchi ya Congo wali anzisha kanisa la ENGLISE EMMANUEL MIRACLE CENTER na sasa litakuwa kanisa la AIC Congo.
Baada ya Utambulisho huo kiongozi wa kanisa la AIC Burundi zamani "kanisa la ENGLISE EMMANUEL MIRACLE CENTER" aliomba kikundi cha Injili na Misheni kufundisha imani ya kanisa la AICT kwa vitendo. Aidha uongozi uliomba kufundishwa, Taratibu za ibada na nyimbo za sifa. Ili kanisa la AIC Burundi lifanane na Kanisa la AIC Tanzania. Pia uongozi wa kanisa la AIC  Burundi umeomba kibari cha kutafsiri nyimbo za sifa, katiba ya AICT, Katekisimu na Taratibu za ibada kwa lugha ya Kirundi wavitumie Burundi. 
Tena, Mwinjilisti kiongozi-Manjondi Ezechiel wa AIC-Burundi, akakiomba kikundi cha Injili na Misheni kuendesha ibada zote wakati wa ziara yao ili viongozi wa AIC Burundi wajifunze kwa kuona na vitendo. 
Pia alisema eneo la kanisa la AIC Burundi zamani "ENGLISE EMMANUEL MIRACLE CENTER" sio la kwao eneo hilo wame pangishwa, hivyo aliwaomba wageni kabla ya kuondoka wafike sehemu inayoitwa "RUBIRA, BUBANZA" waone eneo la kiwanja walilo nunua lenye ukubwa wa " urefu mita 200 na upana mita 100" eneo ambalo watajenga makao makuu ya kanisa la AIC Burundi.
Na ndipo, Mwinjilisti kiongozi-Manjondi Ezechiel akamkaribisha kiongozi wa kikundi cha Injili na Misheni Mwinj. Stephen Kapongo awatambulishe wageni alioambatana nao. Baada ya wageni kumaliza kujitambulisha kwa majina na sehemu walizotoka, Mratibu wa Idara akakubali kuwa wageni wata endesha ibada zote hapo kanisani. Pia wata fundisha masomo yafuatayo:

1. Somo: Imani ya kanisa la AICT- Mwalimu: Mch. Samwel Lupilya
Mch. Samwel Lupilya alikufundisha juu ya Imani ya kanisa la AICT. Pia akafundisha mambo sita muhimu:
 Mungu ni mmoja katika Utatu Mtakatifu (Mt. 3:16-17; 28:19; 15:26)
 Mungu ni Muumbaji na Mlinzi wa vitu vyote...(Mwa. 1:1;26-28)
Uungu na Ubinadamu wa Mungu Mwana, ambaye ndiye Bwana Yesu Kristo aliye Mungu halisi.... (Mt. 1:18-25; Lk. 1:26-38; 2:1-7, 52)
Maandiko Matakatifu ya Agano la Kale na Agani Jipya, yana vitabu 66. (Rum. 3:23; 5:12, 1Yon. 1:8; Zab. 130:3)
Imempasa binadamu kuzaliwa mara ya pili. Yn. (1:12-13; 3:3,5-6)
Kanisa ni watu walioitwa na Mungu kwa njia ya Imani katika Kristo Yesu...(1Kol. 1:2; Yud. 1:1; Efe. 5:20-23; Kol. 1:18)

2. Somo: Taratibu za ibada -Mwalimu: Mch. Emmanuel Makunza
Mch. Emmanuel Makunza wa Dayosisi ya Pwani alifundisha taratibu za ibada za AICT.  Alifundisha juu ya mambo matatu muhimu:
 Viongozi na Wakristo wa hakikishe uwepo wa Yesu Kristo katikati ya ibada zetu.
 Kiongozi ajiandae mapema kabla ya ibada na aongoze kwa utaratibu na heshima.
 Ibada za juma Pili mwongozo wa ibada unasema kabla ya ibada kuanza utulivu uwepo kanisani.

Na baadae  alimkaribisha  Mch. Charles Sanagu kuimbisha wimbo wa sifa no. 5 "Bwana Mungu na shangaa"

Ibada:

Ibada ilianza kwenye kanisa la AIC Buruni saa11 jioni.   Na ibada iliendeshwa na wageni ili kuwapa uzoefu wenyeji wajue taratibu na kanuni za ibada za kanisa la  AIC Tanzania.

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found