HONGERA KANISA LA KILUTHELI

Mimi pamoja na wakristo wote wa Africa Inland Church, Tanzania (AICT) tunawapongeza wakristo wa Kanisa la Kilutheri popote walipo duniani kwa kuishikilia imani ya kweli kwa kipindi cha miaka 500. Kanisa la Kilutheri lilizaliwa mwaka 1517 kwa mwasisi wake, Martin Luther kutongaza rasmi msimamo wa imani inayotegema Maandiko Matakatifu tu. Na pasipo kuongeza ziada, kanisa la Kilutheri ndiyo chimbuko la makanisa mengi yanayotii na kuheshimu maandiko Matakatifu.

Na kwa hapa kwetu Tanzania, tunampongeza sana Mkuu wa kanisa la Kilutheri Tanzania, Askofu Dr Fredrick Onael Shoo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuliongoza kanisa hili kubwa na Maaskofu wote wanao kwa kazi kubwa wanayoifanya. Aidha, tunawapongeza wachungaji wote wa kanisa hili wanaolichunga kundi la Mungu kwa kutumia Maandiko Matakatifu.

AICT inaungana na witu alioutoa Mkuu wa kanisa hili kuwa “wasiache urithi wa imani yao na kukimbilia wapotoshaji wenye lengo la kuwaondoa katika imani kwa Yesu Kristo”.

Mungu, libariki kanisa la Kilutheli

Askofu Silas Kezakubi, Askofu Mkuu, AICT

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found