//social-icons

Askofu Charles Salala Afanya Ziara ya Kikazi Katika Dayosisi ya Tabora photos

Askofu Charles Salala Afanya Ziara ya Kikazi Katika Dayosisi ya Tabora
Askofu Salala na mkewe Mariam pamoja na watumishi Dayosisi ya Tabora wakiwa kwenye hoteli ya Lyamba Wakristo wa kanisa la Mwamapuli wanashangilia kwa furaha kumsindikiza Mchungaji Mteule akawekewe mik Askofu Salala akimwekea mikono Mchungaji Mteule Daniel Malale wa Mwamapuli
Askofu Charles Salala wa AICT Dayosisi ya Pwani, akiwa ameambatana na mkewe, hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi katika AICT Dayosisi ya Tabora. Akiwa katika ziara hiyo, ambayo ilianza December 19, 2015 na kukamilika January 4, 2016, Askofu Salala alibariki na kuwaingiza kazini wachungaji wawili ambao ni Mchungaji Simon Kuhanda wa kanisa la Usevya katika Mkoa wa Katavi, Wilaya ya Mulele na Mchungaji Daniel Malale wa kanisa la Mwamapuli katika Mkoa huo huo na Wilaya hiyo hiyo. Aidha, katika kipindi hicho chote, Askofu alihubiri katika makanisa 12 na kuweka mawe ya msingi kwenye majengo 6. Kiongozi huyo wa kanisa alihitimisha ziara yake kwa kubariki ndoa kumi na moja katika kanisa la Katavi lililoko kwenye mji wa Mpanda Mkoani katavi.